MANAIBU KAMISHINA WA JESHI LA POLISI WALIOKUWA NJE YA NCHI WALA KIAPO CHA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

KIA1
Kamishia wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda akiwaapisha Manaibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP) Modestus Gasper Lyimo na Juma Yussuf (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam. Manaibu Kamishina hao awakupata fursa ya kula kiapo hicho pamoja na wenzao mnamo tarehe 16 Julai 2016.
KIA2
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Kiongozi,Charles Mwankupili akizingumza jambo wakati wa hafla ya kula kiapo cha Maadili kwa Manaibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP) Modestus Gasper Lyimo na Juma Yussuf Ali (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda na Mwakilishi wa IGP, Kamishina wa Jeshi la Polisi Nsato Marijani Mssazya.
KIA3
Manaibu Kamishina Modestus Gasper Lyimo (kushoto) na Juma Yussuf wa Jeshi la Polisi wakila kiapo cha maadili ya viongozi wa umma leo Jijini Dar es Salaam. Manaibu Kamishina hao awakupata fursa ya kula kiapo hicho pamoja na wenzao mnamo tarehe 16 Julai 2016.
KIA4
Manaibu Kamishina Modestus Gasper Lyimo (kushoto) na Juma Yussuf wa Jeshi la Polisi wakitia saini katika fomu za kiapo cha maadili ya viongozi wa umma leo Jijini Dar es Salaam. Manaibu Kamishina hao awakupata fursa ya kula kiapo hicho pamoja na wenzao mnamo tarehe 16 Julai 2016.

MTATURU: JESHI LA POLISI HALIPASWI KUFANYA KAZI KWA MAZOEA

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na askari wa Jeshi la polisi mara baada ya ziara yake katika makao makuu ya Wilaya hiyo eneo la Ikungi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Kituoni hapo.
Dc Mtaturu akikagua chumba cha mahabusu kituoni hapo
Askari watiifu wa Jeshi la Polisi Wilayani Ikungi waliposimama kutoa heshima zao kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi alipotembelea katika ofisi yao

MFUKO KICHOCHEO WA SAGCOT WASAINI MAKUBALIANO NA SHIRIKA LA BOTHAR KUTOKA NCHINI IRELAND

Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCO Bwa. John J. Kyaruzi akisaini makubaliano hayo na Mwasisi wa Shirika la Bothar Bw. Peter Ireton huku wakishuhudiwa na Dkt. Bernard Muyeya (kulia) Mkurugenzi wa Huduma za Nje ya Nchi wa Bothar na Bwa. Abdallah S. Msambachi ( kushoto) Mratibu wa Biashara wa Mfuko wa SAGCOT. 

Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kuongeza tija na uzalishaji kwa
wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani Njombe, Iringa na Mbeya, Mfuko
Kichocheo wa SAGCOT yaani SAGCOT CATALYTIC TRUST FUND tarehe 12 Agosti  2016 umesaini makubaliano na Shirika la Bothar kutoka nchini Ireland
ambalo linajihusisha na kutoa misaada mbalimbali inayolenga kutoa fursa
kwa familia zenye kipato cha chini kuweza kuboresha maisha yao kupitia
uwekezaji wa shughuli zinazowaletea kipato hususani kaya zinazojishughulisha na ufugaji.

Katika makubaliano hayo jumla ya  Ng’ombe wa kisasa 630 wanatarajiwa kuingizwa nchini katika kipindi cha  miaka mitatu. Ng’ombe hao watagawiwa kwa wafugaji walioandaliwa chini ya miradi inayotekelezwa na Mfuko huo, Aidha wafugaji watahakikishiwa  masoko pamoja na huduma mbalimbali za mifugo kupitia wataaalamu wa Halmashauri husika.
Bwa. John. J. Kyaruzi na Bwa. Peter Ireton wakibadilishana hati za makubaliano.

WAZIRI NAPE AFUNGA MASHINDANO YA GOFU YA WAZI YA TANZANIA JIJINI ARUSHA,WAKENYA WATAMBA

Richard Owiti kutoka nchini Kenya akionesha kombe lake la ushindi mara baada kushika nafasi ya kwanza kwa wachezaji wa ridhaa,kwenye mashindano ya Gofu ya Wazi ya Tanzania yaliyoanza kufanyika juzi ijumaa katika viwanja vya Kili Golf-USA River jijini Arusha na kuhitimishwa jana jioni,ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye (wa pili kulia).Kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania (TGU),Joseph Tango wakishuhudia kwa pamoja.Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali jana jioni wakati wa kufunga mashindano ya Gofu ya Wazi ya Tanzania yaliyoanza kufanyika juzi ijumaa katika viwanja vya Kili Golf- USA River jijini Arusha na kuhitimishwa jana jioni,ambapo wageni waalikwa wakiwemo wachezaji wa kulipwa na ridhaa wa mchezo huo walishiriki.PICHA NA MICHUZI JR-ARUSHA

Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akimkabidhi vifaa vya mchezo huo wa Gofu mshindi wa kwanza wa wachezaji wa ridhaa katika Mashindano ya Gofu ya wazi ya Tanzania,Richard Owit kutoka nchini Kenya,yaliofungwa jana jioni katika viwanja vya Kili Golf-USA River jijini Arusha,pichani kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania (TGU),Joseph Tango. Mashindano hayo yaliyokuwa na msisimko mkubwa yalishirikisha washiriki wapatao zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania,Kenya na Unganda.

MSHIRIKI WA MICHUANO YA OLIMPIKI APATA SAPRAIZI YA KUCHUMBIWA BAADA YA KUPOKEA MEDALI

HALI YA TAHARUKI YAUKUMBA UWANJA WA NDEGE WA JOHN F. KENNEDY

TANAPA,NGORONGORO NA IDARA YA WANYAMAPORI SASA KWENDA KIJESHI

Gwaride la wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na maafisa wa Hifadhi za Taifa likiingia katika viwanja vya mazoezi katika kambi ya mafunzo ya Mlele wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akipokea salamu ya utii kutoka kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (hawapo pichani) wakati wa ufungaji mafunzo kwa askari na maafisa hao yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akikagua gwaride wakati wa kufunga mafunzo kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi
Askari na Maafisa wa Hifadhi wakipita kwa heshima mbele ya mgeni rasmi kwa mwendo wa pole na haraka wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu kutoka mfumo wa kiraia.

LIVERPOOL YAIFUNGA ARSENAL NYUMBANI KWAO

ALI KIBA LADY JAY DEE WAFUNIKA TAMASHA LA SEREBUKA 2016 LILILOANDALIWA NA KAMPUNI YA STARTIMES

Alikiba-1
Msanii, Ally Salehe ‘Ali Kiba’ akishambulia jukwaa wakati akitumbuiza kwenye tamasha la kutimiza miaka Miwili ya Chaneli ya Startimes Swahili tokea kuanzishwa Kwake. Tamasha hilo lililopewa jina la Serebuka Festival lililofanyika katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jana ambapo lilidhaminiwa na Kampuni ya Huawei Tanzania.
 Msanii, Snura Mushi, akitumbuiza kwenye tamasha hilo.
Msanii, Juma Kassim ‘Juma Nature, akitumbuiza kwenye tamasha hilo.
 Msanii Stamina akipagawisha kwenye tamasha hilo.
Wananchi wakifuatilia Tamasha la Serebula Festival la kuazimisha miaka miwili ya chanel ya startimes Swahili iliyoandaliwa na kampuni ya Bluelines kwa kushirikiana na uwawei jijini Dare s Salaam jana

TAARIFA RASMI KUHUSU KIFO CHA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI MZEE ABOUD JUMBE MWINYI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa taarifa rasmi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu kifo cha Rais Mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya pili Mzee Aboud Jumbe Mwinyi kilichotokea leo Mji Mwema Dar es Salaam na kuzikwa kesho katika viwanja vya nyumbani kwake Migombani Unguja.[Picha na Ikulu.]15/08/2016.

Kwa masikitiko makubwa, naomba kuwaarifu kuwa, leo tarehe 14 Agosti 2016, Mzee wetu Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia. Kama mnavyofahamu, Marehemu Mzee Aboud Jumbe ni Rais Mstaafu wa Zanzibar awamu ya pili, ambaye vile vile alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Marehemu Mzee Aboud Jumbe amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu kutokana na umri wake.

Msiba huu umetokea nyumbani kwake Mji Mwema, Dar es salaam. Maziko ya marehemu yatafanyika kesho tarehe 15 Agosti 2016 saa 7.00 mchana ambapo maiti yake itasaliwa katika Masjid Mshawar, Mwembeshauri na kuzikwa nyumbani kwake Migombani.

Kufuatia mchango na juhudi mkubwa ambazo marehemu Mheshimiwa Aboud Jumbe Mwinyi alizichukua katika uhai wake kwa kuitumikia, kuiongoza na kuijenga Zanzibar pamoja na nafasi yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nchi yetu imekabiliwa na msiba mkubwa kwa kifo cha kiongozi huyu mahiri.

Kutokana na msiba huu mkubwa kwa nchi yetu, natangaza rasmi siku saba za maombolezo, kuanzia kesho tarehe 15 Agosti 2016. Katika kipindi hicho chote bendera zote zitapepea nusu mlingoti. Kadhalika utaratibu wa maziko utafuata wasia ambao mwenyewe marehemu aliutoa wakati wa uhai wake.

Tunaungana na wanafamilia wote katika kipindi hiki kigumu cha msiba. Naomba kutumia nafasi hii kutoa mkono wa pole kwa wafiwa wote. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie kauli thabit marehemu mzee wetu na amlaze pahala pema peponi, Amin

RAIS DKT. MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA ABOUD JUMBE

ZLATAN IBRAHIMOVIC AJITAMBULISHA KWA GOLI WAKATI MAN UTD IKISHINDA

Zlatan Ibrahimovic amefunga goli katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza wakati Manchester United ikiibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Bournemouth na kumpatia kocha wao mpya Jose Morinho ushindi wa kwanza.

Katika mchezo huo Juan Mata alikuwa wa kwanza kuifungia Manchester United katika dakika ya 40 kufuatia makosa yaliyofanywa na mabeki wa Bournemouth, ambapo baadaye katika dakika ya 59 Wayne Rooney alifunga la pili kwa mpira wa kichwa.

Zlatan Ibrahimovic alijitambulisha rasmi katika Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kufunga goli la tatu kwa shuti la mbali mnamo dakika 64 lililomshinda golikipa, kisha Adam Smith akaifungi Bournemouth goli pekee katika dakika ya 69.
    Juan Mata akifunga goli la kwanza la Manchester United baada ya mabeki kufanya uzembe
   Zlatan Ibrahimovic akiangalia shuti lake aliloachia likielekea wavuni na kuandika goli la tatu
   Mchezaji mpya wa Manchester United Eric Bailly akituliza mpira gambani huku akiwa ameruka juu

Post a Comment

0 Comments